Baada ya kufungia baadhi ya Makanisa nchini Rwanda stori nyingine ninayokusogezea leo March 15, 2018 ni kuhusu marufuku ya matumizi ya adhana (Wito kwa Waislamu kuhudhuria maombi) taarifa hiyo iliyotolewa na serikali ya Kigali imekataliwa na baadhi ya Waislamu nchini humo.
Serikali ya Rwanda katika eneo la Nyarugenge wanakopatikana Waislamu wengi Rwanda wamesema kumekuwepo makubaliano ya kubadili mbinu za kuwaita waumini bila kutumia njia inayosumbua watu.
Tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yanaheshimiwa umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo.
HUDUMA YA KWANZA YA UOKOAJI KWA HELIKOPTA MLIMA KILIMANJARO