Story kubwa ambayo ilichukua headlines siku kadhaa zilizopita ni kuhusu mwimbaji R. Kelly kuiomba Mahakama ya mjini Chicago kumpatia ruhusa ya kwenda mjini Dubai kwa ajili ya kufanya matamasha yake kadhaa ambayo alidai alikubali kutumbuiza kabla ya kutiwa nguvuni.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mail Online umeripoti kuwa Idara ya Vyombo vya Habari mjini Dubai imekanusha kuwa R.Kelly hana onyesho lolote Mjini hapo. Kupitia maelezo waliyotoa wamesema “Mamlaka mjini Dubai haijapokea ombi lolote la onesho kutoka kwa R. Kelly na hakuna ukumbi wowote ambao umewekewa oda (booked)” na waliongeza kwa kusema kuwa R.Kelly hajaalikwa na familia yoyote ya Kifalme.
Wakili wa mwimbaji wa R.Kelly ambaye ni Steven Greenberg amesema kuwa “R Kelly ali-sign mkataba kutoka kwa promoter na kila kitu kuhusu safari kilitoka kwenye mkataba, hatukusema kuwa alialikwa kukutana na familia ya Kifalme mkataba ndio ulisema kuwa akiwa tayari atakutana na familia hiyo”
ULIPITWA NA KILICHOJIRI BUCKETS BAADA YA RC MAKONDA KUSEMA VINYWAJI VIUZWE ‘NUSU BEI’? Bonyeza PLAY hapa chini kutazama.