Club za Azam FC na Mtibwa Sugar ambazo zimekuwa ni club kubwa na alizozichezea marehemu Ibrahim Rajab Juma “Jeba” zimekubali ombi la shirikisho la soka visiwani Zanzibar.
Club hizo zote mbili zimekubali kucheza mchezo wa hisani December 9 uwanja wa Amaan Zanzibar kwa ajili ya kumuenzi mchezaji huyo na pesa zitakazopatikana itapewa familia ya mchezaji huyo.
Hata hivyo Azam FC na Mtibwa Sugar siku ya mchezo huo watauza jezi timu zao zenye jina la “Jeba” kama ishara ya kumuenzi kwa kipekee.