Wizara ya Afya imesema wagonjwa wapya wawili (Watanzania) wamethibitika kuwa na COVID-19 jijini Dar es Salaam, na mmoja kutokea Zanzibar na hivyo kufanya jumla ya wagonjwa waliothibitika nchini mpaka sasa kufikia 6. Watanzania hao walirejea nchini Machi 14 na Machi 17 mwaka huu.