Mahakama ya rufaa nchini Afrika Kusini imemuongezea adhabu ya kifungo mwanariadha mwenye ulemavu Oscar Pistorius kutoka miaka 6 hadi miaka 13 na miezi mitano kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hatua hii inafuatia madai kutoka upande wa serikali kwamba adhabu aliyopewa awali ya miaka sita ilikuwa ndogo. Pistorius alishtakiwa kumuua mpenzi wake kwa kumpiga risasi 4, katika siku ya wapendanao mwaka 2013, na baadaye Pistorious alisema alifyatua risasi hizo kwa kujua ni mwizi.
Familia ya Reeva Steenkamp imeeleza kuwa wamefurahishwa na uamuzi wa mahakama na inaonesha kuwa haki inaweza kuendelea kutendeka nchini humo Afrika Kusini.
Ulipitwa na hii? Muhasibu “Bilionea” wa TAKUKURU alivyofikishwa Mahakamani
Mfanyakazi wa TRA alieishi kifahari na magari 19 kafikishwa Mahakamani.