Hatimaye mwanamitindo maarufu nchini Millen Magese ameonyesha sura ya mtoto wake wa kwanza Prince Kairo na hii ni baada ya kubahatika kumpata mtoto huyo July,2017 baada ya kusumbuka kwa miaka mingi bila kufanikiwa kupata mtoto akisumbuliwa na ugonjwa wa Endometriosis
Kupitia ukurasa wa instagram wa Millen Magese alipost picha ya jarida la Genevive la nchini Nigeria na baadae kufuta ambapo katika jarida hilo linaelezea kuhusu safari ndefu aliyoipitia mwanamitindo huyo mpaka kubahatika kupata mtoto.
Millen Magese alikubali hali yake ya ugonjwa wa endometriosis uliomsumbua kwa muda mrefu na hakuishia kuhangaika mwenyewe bali alitaka ulimwengu mzima utambue kuhusu ugonjwa wa Endometirosis unaotesa wanawake.
Ulipitwa na maneno ya Nay wa Mitego baada ya interview ya Naibu waziri Shonza na XXL