Kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia July 2017 imepungua ikilinganishwa na June 2016 baada ya mfumuko wa bei Tanzania kwa mwezi July 2017 kuonesha umepungua hadi kufikia 5.2% ikilinganishwa na 5.4% ya mwezi June, 2017.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo ameeleza kuwa kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Julai kumesababishwa na kupungua kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula zikilinganishwa katika kipindi cha miezi hiyo miwili.