Rapper Kanye West ambaye pia ni mume wa Kim Kardashian ameweka wazi kuhusiana na Jay Z pamoja na mke wake Beyonce kutoonekana kwenye harusi yake iliyofanyika May 2014 kwamba ni kitendo ambacho kilimuumiza sana.
Rapper huyo ameelezea pia kuhusu uhusiano wake na Jay Z katika mahojiano aliyofanya na Charlemagne tha God na kusema kuwa aliumizwa na kitendo hicho na kuwa Beyonce na Jay Z ni familia yake
“Kiheshima inabidi niseme tu niliumia wao kutokuja kwenye harusi, naelewa walikuwa wanapitia vitu tofauti lakini ni familia hawakutakiwa kukosa harusi”
Leo May 1 Nikkiwapili kaendelea na msimamo wake