Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Magharibi limefanya operesheni maalumu ya ukaguzi wa bidhaa za chakula na vipodozi kwenye maghala, maduka makubwa ya jumla na rejareja, mipakani na bandarini kwa Halmashauri 11 katika mikoa ya Katavi,Rukwa na Kigoma
Akizungumza wakati wa operesheni hii kaimu meneja wa kanda ya magharibi (TBS) Bw. Rodney Alanga alisema lengo la operesheni iliyofanyika kuanzia 2022-02-21 hadi 2022-03-13 lilikuwa kuondoa bidhaa hafifu zinazopatikana katika masoko ya mikoa ya kanda ya magharibi ili kuwalinda walaji/watumiaji wa bidhaa hizi shida ya madhara yanayoweza kujitokeza.
Katika operesheni hii shirika lilibaini makosa yanayofanywa na wafanyabiashara ni kuuza bidhaa za chakula na vipodozi ambazo zimekwisha muda wa matumizi, bidhaa za chakula na vipodozi zisizosajiliwa na TBS, na uuzwaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku kutumika. Aliongeza Bw. Alananga
Katika operesheni hii changamoto kubwa tuliyojifunza ni kwamba wafanyabiashara wengi hupitisha bidhaa njia kwa njia za panya, hununua , kutokagua bidhaa katika maduka yao kuhakiki muda wa mwisho wa matumizi, kutotunza Kumbukumbu za manunuzi na mauzo ya wapi wanenunua na wapi wameuza, na kununua bidhaa za vyakula na vipodozi katika maduka yasiyokuwa vibali au yasiyo sajiliwa na TBS. Alisisitiza Alananga.
Pia TBS imefanikiwa kukamata bidhaa za chakula na vipodozi zenye uzito wa tani 32. 2 na thamani ya TZS 97, 706, 200/= pia inatarajia kufanya uteketezaji wa bidhaa hizo baada ya taratibu zote za kisheria kufuatwa
“TBS imechukua hatua za awali kwa kuzuia bidhaa zote zilizoonekana kuwa makosa ambazo utekelezaji na ufuatiliaji wake utaendelea ndani ya Siku 14 kwa mujibu wa notisi ya kuzuia bidhaa (seizure notice) Amesema Bw. Alananga.
TBS kwa kushirikiana na vyombo vingine vya serikali kama vile Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Mapato, Uongozi wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri itaendelea kufanya Operesheni za kushitukiza ktk maeneo ya masoko mijini, vijijini, mipakani, bandarini na kuwabaini wakiukaji na kuchukua hatua za kisheria ili kulinda afya ya watanzania, biashara na mazingira.
Tunatoa wito kwa wafanyabiashara kuzingatia sheria zilizowekwa ili kuweza kujiepusha na hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na uuzaji wa bidhaa hafifu.