Muigizaji na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu amekuwa ni mtu mwenye kuonyesha majonzi kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na kilio chake cha muda mrefu kuhusiana na kutopata mtoto ambapo amehangaika kwa muda mrefu lakini imeshindikana yeye kuitwa mama.
Kupitia instagram account ya mfanyabiashara maarufu Maznat “Maznat Bridal” anayejishughulisha na make up ameonekana kuona ndoto anayoitamani Wema Sepetu ya kuitwa mama siku moja na hivyo kuamua kumpa moyo kwamba ipo siku na yeye atapata mtoto.
“Kuitwa mama siyo lazima uzae. Ukifikia umri tu wa kuitwa aunt, mama mdogo, shangazi, mama mkubwa ina maana wewe tayari ni mama. Kuwa mama siyo lazima uingie labour, mimi namshukuru Mungu nimezaa na nimelea watoto wangu na wasio wangu”
“Katika yote nimejifunza KUPENDA WATOTO KWA DHATI PASIPO KUBAGUA. Nimejifunza UKIWAPENDA upendo wa kweli huwa wanajua na wao WATAKUPENDA HIVYOHIVYO”
“Lakini zaidi nimeshawahi penda watoto yatima na kujitoa shilingi yangu ya mwisho kuwahudumia angali sikuwahi kuwaona wazazi wao. Tena nikawapenda kwa moyo wangu wote na nguvu zangu zote na wala sikuwa nimewazaa.”
“Mungu ni msiri sana sana mdogo wangu @wemasepetu anajua nini kinamstahili nani, kwa muda gani. Muda wa Mungu ukifika ataku suprise. Atakupa faraja ya ajabu. Atakupa kile moyo wako unahitaji. Atakutunuku zawadi ya kipekee utabaki mdomo wazi ukishangaa maajabu ya Muumba”
“Jipe moyo It is well Eeeh Mungu, kila mwanamke apate katotoo angalau kamoja Amina 🙏🙏 mlale unono. #maznat #maznatbridal#badilimtazamo #amkanamaznat ( nimemuwaza sana Aggy na mtoto wake…nikamuwaza sana Wema. Roho imeniuma…nakuombea sana Wema upate ka kwako Inshaalah🙏🙏🙏)”
Rammy Galis aacha gumzo mitandaoni msiba wa Masogange