Muigizaji Faiza Ally ni miongoni mwa waigizaji waliojitokeza kwenye msiba wa Marehemu Agnes Masogange na ameamua kutoa ushauri kwa waigizaji wa Bongo Movie kuwa na umoja na ushirikiano waliouonyesha katika msiba huo baada ya kumuona Irene Uwoya ambaye alikuwa rafiki wa karibu na Marehemu Agnes kwa kujitoa na kuwa imara.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Faiza Ally ameandika ujumbe huu kwa waigizaji wa Bongo Movie
>>>“Tunaishi kwa kujifunza na mara nyingi mitazamo ya nje sio halisi, naomba nimpongeze @ireneuwoya8 kwa kuwa rafiki mwema a special kipindi hiki , nimemuona akishiriki na kwenye utulivu sana yaani kasimama kama rafiki na hivi ndio inavyo takiwa , yaani jambo linapo kufika la mtu wa karibu sio kulia sana au kupoteza fahamu lzm usimame ujue hatma ya mwenzio kwanza, nampongeza sana”
“@zamaradimketema @stevenyerere2@auntyezekiel @official__husnamaulid_@husnasajent_@shilolekiuno_badgirlshishi@chandeshian_homeaccesories na wengine ambao sikuweza kuwataja kwa kweli mmesimama imara sana , nahisi bongo movie tuna vitu vikubwa sana wote kwa pamoja lkn sijui tunakosea wapi, maana kwa ushirikiano huo huo wa msibani , urudi kwenye kwenye kazi naamini kuna hatua kubwa sana tutapiga ..nisema tu mpo vizuri sana nyinyi ni wa maana sana , uwepo wenu ni muhimu M.MUNGU AWATUNZE 🙏”
Rammy Galis aacha gumzo mitandaoni msiba wa Masogange