Wanajeshi wa kikosi cha kulinda mapinduzi cha Iran wamefyatua makombora kukilenga chombo mfano wa meli zenye uwezo wa kubeba ndege za kivita katika ujia wa bahari wa kimkakati wa Hormuz.
Hayo yamatangazwa na televisheni ya taifa ya nchi hiyo. Mazoezi hayo yana lengo la kuitisha Marekani, wakati kukiwa na mvutano kati ya utawala wa Tehran na ule wa Washington.
Yanadhihirisha pia kitisho cha uhasama wa kijeshi kati ya Iran na Marekani katika ujia huo unaopitisha asilimia 20 ya mafuta yote ya petroli nayouzwa duniani.
Marekani imeyalaani mazoezi hayo ya jeshi la Iran, ikisema ni ya kizembe na kutowajibika.