Michezo

SAFA kuungana na TFF kumuadhibu zaidi Luc Eymael

on

Aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga SC Luc Eymael afungiwa na chama cha soka Afrika Kusini (SAFA) kufanya kazi nchini humo, hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Yanga kumfuta kazi kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi, SAFA pia wamewaomba FIFA na CAF kumuadhibu zaidi ya kocha huyo.

“Tunataka kuonesha mshikamano wetu na sapoti kwa chama cha soka cha Tanzania na Yanga SC, historia yetu, mila na desturi kupinga ubaguzi wa rangi kwa aina yoyote “ taafifa kutoka SAFA

Kama utakuwa unakumbuka vizuri miongoni mwa nchi ambazo amewahi kufanya kazi Luc Eymael na kufundisha club zaidi ya moja ni Afrika Kusini ambapo amewahi kuzifundisha Free State Stars, Polokwane City na Black Leopard.

Soma na hizi

Tupia Comments