Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali za Tsh Biloni 3.6 inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Godfrey Gugai na wenzake hadi December 4, 2017.
Mbali ya Gugai, Washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera ambapo hatua ya kuahirishwa kwa kesi hiyo inatokana na mvutano wa kisheria baina ya upande wa mashtaka na utetezi ambao ulitaka mashtaka ya utakatishaji fedha yaondolewe.
Kutokana na mvutano huo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi December 4,2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi ambapo Washtakiwa wamerudishwa rumande wakikabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.
Ulipitwa na hii? Mfanyakazi wa TRA alieishi kifahari na magari 19 kafikishwa Mahakamani.
BREAKING: TAKUKURU ilivyotangaza kumtafuta huyu Mtanzania mwenye pesa na mali nyingi, bonyeza play hapa chini kuona ilivyokua