Mix

Umeipata hii ya joto kali lililoyeyusha mpaka gari? Nimeisogeza toka Italy… (+Video)

on

italy

upande mmoja wa gari hili ukiyeyuka.

Stori za joto kuongezeka kipindi hiki sehemu mbalimbali duniani zimekuwa zikichukua headlines kubwa sana, ilianza Dubai joto lilipanda mpaka nyuzi 38, tukasikia Uingereza nako nyuzijoto liligonga 40 ikaja India pia joto kufikia nyuzi 45.

italy2

bampa ya nyuma na taa vikiyeyuka pia..

Nimekutana na sotri kutoka Italy ambako nyuzijoto limeongezeka kufikia nyuzi 37 Centigrade.. matukio na athari za jua yamekuwa yakiweka headlines mbalimbali Italy moja wapo ni hii ya gari kuyeyuka kutokana na joto kali la jua.

Tukio lilinaswa kwenye picha na video na mtalii mmoja aliyekuwa anatoka hotelini kuelekea beach na kisha kushangazwa kuona uji uji mzito unadondoka kutoka kwenye gari hilo, alipolikaribia gari hilo aligundua kuwa gari lilikuwa linayeyuka kutokana na joto kali la jua.

italy3

Kitu hiki kimewashangaza watu wengi huku vyombo vingi vya usalama nchini humo vikitahadharisha watu kupunguza kutoka nje na kwenda baharini, kingine wameshauriwa kufunga viyoyozi vitakavyowasaidia kupunguza joto.

Hapa chini nimekuwekea kipande cha video kinachoonesha gari hilo likiyeyuka.


PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments