Jana kulikuwa na Kikao cha Umoja wa Vyama vya UKAWA, lakini katika Kikao hicho hakukuwa na Kiongozi yoyote wa CUF, mitandaoni kukaanza kutembea uvumi kuhusu kutokuwepo kwao.
Nilikutana na #Tweets kwenye ukurasa wa Gazeti la MWANANCHI ambazo walikuwa wamemnukuu Kiongozi wa CUF Magdalena Sakaya kuhusu sababu za CUF kutokuwepo.
Stori imeingia kwenye Headlines tena kwenye habari ya ITV kuhusu ishu hiyo, July 11 2015 Professa Lipumba alisema kwamba CUF watamtangaza mgombea wao July 14 2015 lakini haikuwa hivyo.
>>>> “Professa Lipumba alisema hivyo baada ya kujua kwamba tutakaa na Viongozi wengine tufikie maamuzi lakini ikatokea tofauti kabisa… Sisi ndani ya CUF hakuna Kiongozi yoyote mwenye mamlaka ya kuamua tatizo gumu ambalo linatakiwa kuamriwa na Kikao husika, hata mimi naweza kufukuzwa muda wowote kama nikikiuka taratibu kama hizo…“>>>> Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu CUF Tanzania Bara.
Kwenye Kikao cha Viongozi wengine wa UKAWA waliokutana jana walisema tayari wamempata Kiongozi wa kuwakilisha UKAWA japo CUF hawakushiriki Mkutano huo >>> “Kwa mashauri tuliyoyafanya, tumefanikiwa kwa njia ya maridhiano kumpata Mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya UKAWA kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015…” >>>> James Mbatia.
MZEE KINGUNGE KUHUSU MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM.
Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru amekuwa mmoja ya Wanachama wa CCM ambao wamejitokeza kupinga utaratibu uliotumika kumpata Mgombea wa CCM siku chache baada ya Chama hicho kumtangaza Mgombea wa Urais wao kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
>>> “Kitendo cha kuinyang’anya Kamati Kuu kazi yake sio cha kawaida, ni uvunjifu wa taratibu na hakuna uadilifu ndani yake… Kamati ya Maadili yenyewe inavunja maadili, maadili ya Chama yananzia kwenye kuheshimu muundo wa Chama na taratibu zake” >>>> Mzee Kingunge.
Mzee Kingunge anapinga pia kuhusu utaratibu uliotumika kumpata Mgombea wa Urais >>>> “Kamati Kuu inapelekewa orodha ya watu watano wapitishwe, hawa Wagombea wote 38 waliorudisha fomu hawakuwaona, hawakupita mbele yao, hawakuwauliza maswali na hata kwenye Kamati ya Maadili naamini hawakuitwa.. Kuna watu wachache wamekaa wakatengeneza orodha yao” >>>> Mzee Kingunge.
Kingine ni hiki alichokisema kuhusu Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa >>>> “RICHMOND imempa ushindi Lowassa, kwa sababu Serikali yenyewe imekiri hakuna lililoharibika pale, yeye aliwajibika kisiasa.. ndani ya Bunge kulikuwa na kundi kubwa nia yao ni kumchafua Edward kwa sababu zao Kisiasa.” >>>> Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru.
Nilirekodi stori zote kwenye Habari #ITV, unaweza kubonyeza play hapa kuzisikiliza.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.