Baadhi ya mastaa wamendelea kuguswa na taarifa za kifo cha mwanafunzi Aquillina Akwilini aliyepigwa risasi kifuani siku ya February 16,2018 na Polisi na wameonyesha hisia zao kupitia mitandao ya kijamii akiwemo Diamond Platnumz, Roma Mkatoliki.
“Umekufa Kipindi Cha #MweziWaToba Tena Ni Ijumaa Ya Kwanza Ya #NjiaYaMsalaba Damu Iliyomwagika Msalabani Ni #AganoKwetu!! A SINGLE #BULLET MAY CAUSE MAJOR #NEGATIVITIES#NAWAZA”
“Pengine Ulikuwa Na Ndoto Za Kuja Kuwa Kiongozi Bora Kwa Taifa!!
Ndoto Zimezima Kama Mshumaa!!Pengine Wazazi Wamewekeza Kukusomesha Ili Uje Kuwa Msaada Kwao Ukihitimu Chuo!! Nani Sasa Atawasaidia!?”
“Pengine Risasi Ile Ingeweza Kumpata Hata Mtoto Wangu Mimi Au Mtoto Wako Wewe Unayesoma Ujumbe Huu. Ambaye Hana Hatia!! Pengine Zinaweza Kuwa Nyingi Sana Lakini Ukweli Ni Kwamba#UmetulizaWengi_Aquiline Kapumzike Mdogo Wangu!!” #RIP My Condolences To The #Family #NIT#Friends
“Mwenyez Mungu aipe Nguvu familia ya Marehem na Kuilaza Roho yake Mahala Pema peponi Amin….🙏
Diamond na Roma walivyoguswa na kifo cha mwanafunzi aliepigwa risasi
Marehemu Aquilina alikua kwenye mpango wa kuanza mazoezi kwa vitendo