January 12, 2020 Mwanamke mmoja nchini Uganda amekamatwa akiwa amebeba vipodozi haramu ambavyo alikuwa amevifunga na kuvivalisha nguo ili aonekane kuwa amebeba mtoto mdogo.
Kamishna wa Bidhaa nchini humo, Dickson Kateshumbwa, amenukuliwa akisema, “Mtoto ghushi alipandishwa gari la kutoka Congo katika kituo cha Mpaka wa Mpondwe, na baadae iligundulika mtoto huyo kuwa ni Mwanasesere aliyekuwa amesakamiwa vipodozi haramu, baadhi ya walanguzi huendelea kushangaza”.
Aidha, Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA), imesema mbinu hiyo ya usafirishaji tayari inafahamika, hivyo ni vigumu kupitisha vipodozi bandia nchini humo.
Vipodozi Haramu vilipigwa marufuku nchini Uganda mwaka 2016 kutokana na utafiti kuonyesha kuwa, viwango vya madini ya Zebaki na Hydroquinone vina Madhara Kiafya.
ASKARI AKAMATWA AKIPOKEA RUSHWA YA MILIONI 1.5 ILI ATOE DHAMANA