Jumapili Septemba 11 2016 waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye kwa niaba ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa amezindua rasmi matumizi ya tiketi za kielektroniki katika uwanja mkuu wa taifa.
Mfumo huo ni agizo la waziri mkuu Majaliwa kuhusu udhibiti wa mapato kwenye viingilio vya mlangoni ambapo ni mfumo utakaomtaka shabiki kuwa na kadi mfano wa zile za ATM ambapo atakuwa na uwezo wa kadi yake aliyopewa kufanya manunuzi/malipo akiwa pia na uwezo kununua tiketi za mechi atazopenda kupitia kadi hiyohiyo.
Miongoni mwa waliopewa kadi za kuingilia uwanjani ni waziri Nape, Rais Magufuli na makamu wake mama Samia Suluhu ikiwa ni uhamasishaji ambapo smartcard hiyo ya kukuwezesha kuingia uwanjani itatolewa bure kwa shabiki na baada ya hapo ataanza kuingia nayo uwanjani baada ya kuiwekea pesa.
Faida nyingine ya mfumo huo ni kuwa hakutakuwa tena na utaratibu wa kugawanya mapato kwa njia ya mkono kwenda katika taasisi husika ila ukikata tiketi asilimia za mgawanyo zitakuwa zinafanywa kiteknolojia zaidi kwenda TFF, TRA, BMT na sehemu nyingine zinazohusika.
MANENO YA WAZIRI NAPE KUHUSU UUZWAJI NA UKODISHWAJI WA VILABU VYA SIMBA NA YANGA