Mkali kutoka Kenya ambaye hivi sasa anamiliki headlines kutokana na wimbo wake wa ‘Kioo’, wakati watu wengine wakiungana na familia zao kusherekea sikukuu ya Pasaka yeye alitafuta njia ya pekee kusherekea siku hiyo.
Jaguar zaidi ya muziki ni msanii aliyefanikiwa sana kwenye uwekezaji ambao unamfanya kuwa mmoja kati ya wasanii wanaotengeneza pesa nyingi sana nje ya muziki hadi kumiliki ndege yake binafsi.
Siku ya Pasaka Jaguar alienda kwenye gereza ambalo ali-shoot video yake ya Kioo na kuwafanyia party ya bure wafungwa hao.
Jaguar anasema kwamba ameamua kuwafanyia thanks giving party siku hiyo ya Pasaka kwa kuwashukuru kwa kile walichokifanya kwenye video ya Kioo na kuifanya ifanikiwe hadi sasa.
Hizi ni video mbili kutoka kwa Jaguar akiwa kwenye show hiyo