Hizi stori ziko nyingi sana zinazohusu wazazi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watoto wao, wako wanaoenda mbali zaidi na kufanya ukatili kama wa kubaka na kulawiti watoto pia.
Imenifikia hii kutoka Zimbabwe, baba kambaka mtoto wake na kwenye kujitetea anasema kwamba eti ni utaratibu na utamaduni wao kutembea na mtoto wa kwanza ndani ya familia.
Polisi hawakumwachia, mzee huyo amefunguliwa mashtaka kwa kosa la ubakaji lakini bado alichoendelea kujitetea ni maneno yake yaleyale kwamba huo ni utamaduni wao kabisa !!
Wazazi wa mtoto huyo walitengana, siku ya tukio binti aliamua kwenda kumsalimia baba yake… baba huyo akavamia ndani ya chumba cha mtoto huyo na kumbaka.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.