Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linamshikilia mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Abraham Obed (55) mkazi wa Kata ya Isanga jijini Mbeya kwa tuhuma za kughushi mihuri 66 ya taasisi mbalimbali ikiwemo ya Jeshi hilo, Mahakama na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Disemba 31 mwaka 2019 saa 11:00 jioni katika Mtaa wa Sokoine katika Kata ya Sisimba.
Amesema Jeshi hilo lilipata taarifa za siri kutoka kwa baadhi ya wananchi jijini humo wakimtuhumu mtuhumiwa kwa kugushi mihuri hiyo na kisha kuitumia kwa ajili ya kutengeneza nyaraka bandia kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
NAIBU WAZIRI AGUNDUA MCHEZO MCHAFU NIDA, APIGA MARUFUKU MAWAKILI