Nadal Abubakary ni kijana aliyewagusa watu wengi mtandaoni baada ya video’s zake kusambaa zikimuonesha akiwa na ulemavu wa Miguu baada ya kuumwa Ugonjwa ambao haujajulikana mpaka leo hii.
Nadal ambaye alianza kusumbuliwa na Ugonjwa wa miguu baada ya kudondoka wakati alipokuwa kwenye mishe mishe zake za kutafuta Maisha Kariakoo akisimamia Duka la Mama yake, amesema haelewi ni Ugonjwa gani unamsumbua kwani kashafanya vipimo na bado Madaktari wameshindwa kugundua.
Kwa sasa amekuwa akiendelea na Mazoezi ambayo yamekuwa yakimgharimu kiasi cha ELFU 36 kila siku kitu ambacho kimemfanya ashindwe kuendelea kwa miezi mitatu kutokana na familia yake kutokua na uwezo wakuendelea kulipia gharama.
Ayo TV ilifanikiwa kufika mahala anapoishi Nadal aelezea kile kilichotokea mpaka kuwa katika hali hii sasa, unaweza ukabonyeza play kumsikiliza