Vijana watatu wakazi wa Sumbawanga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kusambaza ujumbe wenye lengo la upotoshaji kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria Leticia Sasabo kwa nia kujipatia fedha kutoka kwake kinyume na sheria.
Washtakiwa hao ni Japhet Mzuri, Joseph Richard na Justin Kapita ambao wote ni wakazi wa Sumbawanga mkoani Rukwa
Wakisomewa hati ya mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Rashid Chaungu amedai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja wametenda kosa hilo January 18 mwaka huu wakiwa Sumbawanga.
Wakili Simon amedai kuwa katika tarehe hiyo washtakiwa hao walituma ujumbe unaosomeka “Chukua namba hii ndio utumie kutuma hiyo pesa 0757-648067 jina litatoka Mwamalekela” wakati wakijua ni kosa kisheria.
Baada ya washitakiwa hao kusomewa shtaka linalowakabili wote wamekana kufanya kosa hilo na kuomba dhamana.
Wakili Simon amedai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kwamba upande wa mashtaka hauna pingamizi na dhamana hivyo kuomba mahakama hiyo kuweka masharti yatakayosababisha watuhumiwa kufika mahakamani bila kukosa.
Hata hivyo Hakimu Chaungu ametoa mashrti ya dhamana ambapo kila mshitakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wakazi wa DSM watakaosaini bondi ya shilingi milioni kumi kila mmoja.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi mach 23 mwaka huu itakapotajwa na washtakiwa wamepekekwa gerezani.
BREAKING: ALIEWAHOJI MEMBE, KINANA (MANGULA) AWEKEWA SUMU ALAZWA “HATA AWE WA CCM TUTAMKAMATA”