Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Mapinduzi ya Zanzibar inaweza kuwa sbb kubwa katika sababu za kuungana na Tanganyika; kulinda amani na utulivu, pia kuharakisha maendeleo.
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 12, 2015
Pamoja na kuwakumbuka wanamapinduzi, na waasisi wa Uhuru wa Tanganyika na Muungano wetu, tutafakari kuudumisha zaidi na kuulinda UTanzania!
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 12, 2015
“Huwezi kuwa mwana wa nchi ikiwa huna uchungu wa nchi yako, ni wajibu kuitetee na kuipigania. Huo ndiyo utu&Uzalendo. pic.twitter.com/lmYfY28FI8
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 12, 2015
Kheri ya Siku ya Mapinduzi kwa Watanzania wote Bara na Visiwani. Umoja wetu ndio silaha yetu Daima…tusimame Imara… #Miaka51YaMapinduzi
— Bernard Membe (@BernardMembe) January 12, 2015
Niwatakie kila la kheri na furaha watanzania wenzangu tunaposherehekea siku ya Mapinduzi.Mapinduzi Daima! @jmkikwete @BernardMembe
— Jamal Malinzi (@jamalmalinzi) January 12, 2015
Hivi hii tabia ya mvua nyesha na umeme ukatwe ni kuendekezwa?ama?….kila mvua ikinyesha basi lazima wenye umeme wao watakata arrrrrrrrghrgh
— Mwasiti Almas (@mwasitiJ) January 11, 2015
Baada ya kupumzishwa na AMIRÎ JESHI MKUU…pasi CHUKULIWA hatua yoyote. PROF yuko JIMBONI(peku)!!#BringBackOurMoney pic.twitter.com/3uM8RwawiW
— Halima James Mdee (@halimamdee) January 12, 2015
Machozi, jasho na damu ya wote walioshiriki mapinduzi ya Zanzibar yasiende bure.Tuikumbuke siku hii kwa kuenzi kile walichopigania.
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 12, 2015
Unapokua unafuata uelekeo wako kuna watu wata-Kukusindikiza katika Safari yako, wengine watakusaidia Mizigo yako, Ila sio wote watafika nawe
— Nisher (@NiSHER_) January 12, 2015
Niko Kenya line yangu iko off but nashangaa huko Tanzania iko ON na inatumika
— Ambwene AY (@AyTanzania) January 12, 2015
Kuna mtu amehack namba yangu ya Tigo anaomba watu pesa
— Ambwene AY (@AyTanzania) January 12, 2015
Blog:
Saleh Jembe: YANGA SASA YAWASHITAKI FIFA JAJA, KASEJA NA OKWI
Klabu ya Yanga imechukua uamuzi wa kuwashitaki wachezaji watatu moja kwa moja kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Yanga imetangaza kuwashitaki kipa Juma Kaseja, kiungo Mganda Emmanuel Okwi na mshambuliaji Jaja raia wa Brazil.
Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Frank Chacha amesema leo wamechukua uamuzi huo kutokana na wachezaji hao kukiuka vifungu vya sheria.
“Lakini pia tutaishitaki Simba kwa kuhusika kuvunja vifungu vya kisheria kutokana na kumshawishi Okwi kuvunja mkataba wetu,” alisema Chacha.
Jaja:
Yanga inasema alishindwa kurejea nchini kwa madai ana matatizo ya kifamilia. Lakini wanashangazwa kuwa hajarudi hadi leo na kuna taarifa amepata timu nyingine, hivyo wanashitaki.
Okwi:
Amekiuka sheria kwa kuvunja mkataba, wanaamini hakuwa sahihi na pia Simba ilimshawishi kuvunja mkataba nayo wanaishitaki.
Kaseja:
Alishindwa kufuata vipengele vya kikatiba ikiwa ni pamoja na kutokwenda mazoezini wanadai bila ya kuwa na taarifa yoyote.
BBC Swahili: Messi:”Tetesi za kuhama ni porojo tu”
Mchezaji mahiri, Lionel Messi anasema kuwa atasalia katika klabu ya Barcelona baada ya kukanusha umbea wa watu kwamba yuko njiani kutoka Barceola.
Messi ambaye ni mshambuliaji wa Barcelona anasisitiza kwamba hataki kuondoka Barca na kusema madai kwamba alimtaka kocha Luis Enrique, kupigwa kalamu ni porojo tupu.
Taarifa za awali zilisema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitaka sana kuondoka katika klabu hio kufuatia tofauti kati yake na kocha Enrique.
“sina nia ya kuondoka na kuhamia klabu yoyote kama vile Chelsea au Man City,” alisema Messi baada ya kuhakikisha timu yake ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Atletico Madrid.
“nimechoshwa sana na umbea wa watu. Sikutaka klabu kumfuta kazi mtu yeyote. ”
Messi, ameteuliwa kuwania tuzo ya mcherzaji bora zaidi duniani, amekuwa akicheza Nou Camp, kwa miaka mingi huku akipata akishinda mataji mengi.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook