Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Yaliyoandikwa kuhusu Mimi na Kingunge ni uzushi wa kutunga na Hakuna ukweli wowote. Sijaongea wala kujibizana na Mzee Kingunge kuhusu Urais
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 14, 2015
Kesho asubuhi nitatembelea JKIA kujionea adha wanayoipata wafanyabiashara waTanzania wanaopeleka wageni uwanjani hapo kabla ya kumwonaWaziri — Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 14, 2015
Kamati Kuu imejadili: 1.SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW 2.WALIOPEWA ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI 3.SOKO LA MAHINDI 4.RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW CCM imesikitishwa na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo — Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW: i) Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
ii)Kamati Kuu imewataka wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika, wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha. — Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
iii)Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
iii) Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la kamati kuu juu ya wahusika wa Escrow. — Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
2 WALIOPEWA ADHABU. Itakumbukwa makada 6 walipewa adhabu kwa ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
2. ADHABU Baada ya muda wa adhabu kuisha, itafanyika tathmini kuona kama walizingatia masharti,ambao hawakuzingatia wataongezewa adhabu. — Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) January 14, 2015
Tumejibu maswali yote yanayoulizwa mara kwa mara na kuelezea dira na ajenda mpya kwa mapana na marefu. pic.twitter.com/jtcpT4z98c
— January Makamba (@JMakamba) January 14, 2015
Kwa mujibu wa mwandishi, kitaanza kuuzwa leo mitaani na madukani na jioni ya leo kitaanza kupatikana mitandaoni. pic.twitter.com/ZpLph0itM7 — January Makamba (@JMakamba) January 14, 2015
Kwa niaba ya Padre Karugendo, namshukuru sana Mzee Mwinyi, Rais Mstaafu, kwa kuandika dibaji yenye maneno maridhawa. pic.twitter.com/IJOt5FU1t8
— January Makamba (@JMakamba) January 14, 2015
Facebook
CloudsFM:
DAZ BABA AKANA KUTUMIA ‘UNGA’
Wiki iliyopita ilisambaa picha ikimuonyesha msanii wa Bongo Fleva aliyekuwa mmoja wa mwanamuziki wa kundi la Daz Nundaz, Daz Baba amechoka na kuonyesha kuwa anaumwa na anahitaji msaada.
Msanii huyo amezungumza na XXL na alisema kuwa amesikitishwa na taarifa hizo kwani ni uzushi na kwamba yeye ni mzima haumwi na akizungumzia ishu ya kutumia unga alikana kutumia madawa ya kulevya.
Blogs
BBC:RBaundi ya pili taifa Cup wanawake Jumamosi
Mechi za kwanza za raundi ya pili ya mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake-Tanzania (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa wikiendi hii (Januari 17 mwaka huu) kwenye miji minane tofauti nchini.
Timu tisa zilizofuzu kutoka raundi ya kwanza baada ya mechi za nyumbani na ugenini akiwemo mshindwa (best loser) zitaungana na Ilala, Kinondoni na Temeke kucheza raundi ya pili. Mechi za marudiano za raundi hiyo zitachezwa Januari 21 mwaka huu.
Hatua ya robo fainali itakayochezwa Januari 26 na 27 mwaka huu pamoja na nusu fainali na fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Proin Promotions itafanyikia jijini Dar es Salaam.
Saleh Jembe
TFF YAFUNGUA MAKUCHA, POLISI MARA YAZUIWA KUCHEZA UWANJA WA KARUME MUSOMA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeizuia timu ya Polisi Mara kutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na matukio ya vurugu na uvunjifu wa amani ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za FDL zinazochezwa kwenye uwanja huo, ikiwemo ile ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga ambapo waamuzi walipigwa.
Kamati zinazohusika zitakutakana hivi karibuni kupitia matukio yote ya utovu wa nidhamu kwenye FDL, na hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ikiwemo na viwanja ambavyo vimekuwa na sifa ya vurugu.
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vina wajibu wa kutoa ulinzi wa kutosha viwanjani wakati wa mechi.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> > twitter Insta Facebook