Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Ni mwaka kamili leo tangu nilipoapishwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Taifa liko vitani dhidi ya majangili na mtandao wa uhalifu
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 20, 2015
Niliagiza kufanyika sensa ya Tembo na Faru kote nchini ili tujue rasilimali ya viumbe hawa ni wangapi ikiwa ni hatua ya kuweka uwazi takwimu — Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 20, 2015
Natarajia kutangaza kwa dunia matokeo ya sensa ya Tembo na Faru nchini katika kipindi kifupi kijacho na hatua zaidi tunazozichukua kunusuru
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 20, 2015
Sku hizi Kuna status za Niko single ila nina mtu. — Noorah (@BabaStylz) January 20, 2015
Zitto Kabwe: Kura ya maoni ya Katiba ifanyike baada ya uchaguzi Mkuu. Naungana na Jaji Warioba na Prof. Lipumba katika hili. Mwaka huu tuchague Viongozi tu
2. PAC imemaliza mahojiano ya siku 2 na TRA ( mamlaka ya Mapato ). Mambo mengi tuliyoagiza yamefanyiwa kazi. Misamaha ya Kodi na ukwepaji Kodi bado ni tatizo kubwa sana. Tarehe 22 January 2014 PAC itapokea Taarifa ya ukaguzi Maalumu wa misamaha ya kodi
3. Wasanii wamelipa kodi ya tshs 348 milioni katika miaka 2 ( 2012/13 na 2013/14 ) tangu urasmishaji wa Kazi za wasanii uanze. Jumla ya kazi 8m zilisajiliwa kipindi hicho, wastani wa kazi 11 kila siku.
Chanzo: taarifa ya TRA kwa PAC January 2015
CLoudsFM: JAY MOE ASHINDWA KUTOA ALBAM KISA KUKOSA MWAMKO WA ALBUM ZA BONGO FLEVA HIVI SASA.
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Jay Moe,ambaye alikuwa kimya kwa kipindi kirefu mara ya mwisho alikuwa na deni kwa mashabiki wake la Mchongo wa deni la Album ya Mocumental. Album hiyo ilikuwa itoke zaidi ya miaka 3 iliyopita yaani kabla hata album hazijaanza kubuma kuuzika,Jay moe kila alipokuwa akiiulizwa kuhusu albam hiyo hakuawa na majibu sahihi lakini ameamua kufunguka kuwa sababu ni kukosa mwamko katika uuzaji wa albamu za muziki wa Bongo Fleva.
Blog
Mwananchi: Mutabingwa wa Escrow apata dhamana
Meneja Misamaha ya Kodi TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa anayekabiliwa na kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh 1.6 bilioni kutoka akaunti ya Tegeta Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ameachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Hakimu Mkazi, Frank Moshi jana alimuachia huru Mutabingwa baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwasilisha fedha taslimu Sh 1bilioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
Mutabingwa aliachiwa huru kwa dhamana baada ya kuwasilisha hati tano za nyumba za watu mbalimbali zenye thamani ya Sh 1.332 bilioni, wadhamini watatu ambao kati yao wawili walikuwa wafanyakazi wa TRA na mmoja mjasiliamari.
Kila mdhamini kati ya wadhamini hao, kila mmoja alisaini hati ya dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh340 milioni na mshtakiwa huyo aruhusiwi kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.
Baada ya kukamilisha masharti hayo ya dhamana, Hakimu Moshi alimuachia huru mshtakiwa huyo na akaiahirisha kesi hadi Januari 29,2015 ambapo mshtakiwa huyo atasomewa maelezo ya awali (PH).
Awali akisomewa hati ya mashtaka inayomkabili mshtakiwa huyo alidaiwa kuwa alitenda makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1)(a) cha sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai akimsomea mashtaka hayo yanayomkabili mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda kuwa Januari 27, 2014 katika Benki ya Mkombozi wilaya ya Ilala , alipokea Sh1.6 bilioni kupitia akaunti namba 00110202613801.
Swai alidai kuwa mshtakiwa huyo akiwa katika Benki ya Mkombozi alijipatia kiasi hicho cha fedha ambacho ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow na kwamba alizipokea kutoka kwa James Burchard Rugemalira ambaye ni Mshauri huru wa Kitaalam, Mkurugenzi wa VIP Engineering na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits ambayo ni mali ya Rugemalira mahakamani kitu ambacho ni kinyume cha sheria.
Jaji Warioba: Rais ajaye anafahamika
Dar es Salaam. Wakati Taifa zima likiwa katika kitendawili cha kumjua kiongozi wa nchi atakayepatikana baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Rais ajaye anafahamika.
Akizungumza katika mahojiano maalumu jana, Jaji Warioba alisema si kazi ngumu kwa Watanzania kumfahamu rais ajaye kwa kuwa katika miaka 50 tangu tupate uhuru, Watanzania wanazijua sifa za kiongozi bora.
Jaji Warioba alisema; “Tatizo la kumjua rais afaaye tunalikwepa lakini linafahamika. Wanaotumia fedha na lugha chafu katika kampeni na hao ndiyo wasiotakiwa.”
“Katika miaka 50 tunazijua sifa za kiongozi bora. Hapa tunakwepa tatizo tu. Tatizo ni matumizi ya fedha na lugha chafu katika kampeni,” alisema Jaji Warioba ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu.
Hadi sasa wanasiasa zaidi ya 20 wakiwamo wa CCM na upinzani wamekuwa ama wanatajwa au wameonyesha nia ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Ukiacha wale wanaotajwa, wanasiasa waliotangaza nia hiyo kutoka CCM ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, huku Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed akitangaza nia kupitia ADC.
Akifafanua zaidi, Jaji Warioba alisema kila mtu anaweweseka kuhusu kiongozi anayefaa ingawa ni kazi rahisi kumjua kutokana na ujuzi tulionao wa miaka zaidi ya 50 ya uhuru.
Kadhalika, Jaji Warioba alisema viongozi wa Serikali hawana budi kuangalia taswira ya uchaguzi mkuu ujao kupitia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao umeonekana kuwa na kasoro zilizosababisha vurugu.
“Nchi hii ina amani na tujitahidi kuilinda amani yetu. Katika uchaguzi huu tufanye kila tuwezalo kuweka maandalizi yenye umakini,” alisema Warioba na kuongeza: “Nasisitiza amani. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni funzo.”
Tetesi kuwania urais
Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari, likiwamo gazeti la chama tawala, viliripoti tetesi kuwa Jaji Warioba anaandaliwa kuwania urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), tetesi ambazo kiongozi huyo alizikanusha vikali.
Ni halali yako kupata kila kinachonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta Facebook