Kupitia mitandao mbalimbali mchini Uingereza imeripoti kuwa penzi kati ya mwimbaji Adele pamoja na mume wake Simon Konecki limeisha baada ya kudaiwa kuwa wawili hao waliachana kwa suivi mkubwa mwaka 2018.
Adele pamoja na mume wake walidumu kwenye ndoa tokea mwaka 2016 huku ikiripotiwa kuwa walidumu kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa miaka saba na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.Imeelezwa kuwa Simon ana uwezo wa kupata nusu ya utajiri wa Adele ambao unatajwa kufikia £uro Milion 150 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 450 za Kitanzania.
Inaelezwa kuwa Adele aliwahi kuuza nyumba ya kifahari iliyopo Uingereza mwezi February, 2019 aliyokua akiishi na mume wake yenye thamani ya Euro milion 3 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 7 za Kitanzania na kuziingiza pesa hizo kwenye akaunti ya mume wake Simon.
Inatajwa kuwa Adele kwa sasa amebakiwa na nyumba nyingine tatu ambapo moja inatajwa kuwepo mjini Beverly Hills Marekani, nyingine ipo Kensington na ya mwisho ipo Southwest London.
AUDIO: FAIZA ALLY AWAKANA WATOTO WAKE KISA MPIGA PICHA “NYIE WASHAMBA HAWAKO HIVI”