Bongo tunaita muziki wetu wenyewe Bongo Fleva, ukifika Nairobi unaambiwa wao wana Genge, muziki ambao tumeusikiliza ukisafiri kwenye njia moja ya burudani Afrika Mashariki na hii Bongo Fleva, Jua Cali ni mmoja ya Wagenge ambao wamesafiri safari ndefu sana na hii Genge.
Safari hii mgenge kajipanga, anakuja na Single inayoisimulia Nairobi yao yani, unaambiwa humo ndani kuna message muhimu hata kwa mgeni anayeingia Nairobi kwa mara ya kwanza, itamfanya awe macho na mishemishe za hapo town.
‘Karibu Nairobi‘ ni ngoma ambayo hapo ndani kuna mistari yenye mengi kuhusu Nairobi.
Teaser ya kichupa hicho ameshare na sisi kwenye ukurasa wake Instagram halafu ameandika “KARIBU NAIROBI’ VIDEO dropping kesho @3PM sharp” @juacaligenge
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook