Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa muigizaji na muimbaji Jennifer Lopez amefanya kitu cha utofauti ili kuchangia wahanga wa kimbunga nchini Puerto Rico kilichotokea 2017 na kuwaacha maelfu ya watu bila makazi.
Jennifer Lopez amepanga kuuza mavazi yake ya polisi aliyowahi kuyatumia katika tamthiliya ya “Shades of Blue” miaka kadhaa iliyopita pamoja na vitu vingine vikiwemo funguo za gari ya polisi, kitambulisho cha FBI, files zilizotumika katika tamthiliya hiyo.
Mwanamuziki huyo anashirikiana na kampuni ya Hispanic Federation, UNIDOS Disaster Relief and Recovery Program ambapo amepanga kuvipiga mnada vitu hivyo kuanzia September mwaka huu ikiwa kiwango cha ununuzi kitaanzia dola 25 za Kimarekani sawa na Shillingi elfu 57 za Kitanzania na kuamini hela hizo zitasaidia watu waliokutwa na maafa hayo ya kimbunga.
EXCLUSIVE: Fundi aliyepiga Ganun wimbo wa Alikiba