Leo December 29 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ametembelea ujenzi wa makazi ya viongozi wa wilaya wa Ikungi mkoani Singida ambapo amewashukia Wakala wa Majengo nchini ( TBA) kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali waliyopewa na Tawala za Mikoa na Mamlaka za serikali za Mitaa(TAMISEMI).
Jafo ameonyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa TBA alipotembelea wilayani hapo ambapo muda uliopangwa kukamilisha kazi hiyo umeshapita huku kazi ikiwa bado haijakamilika ambazo zinagharimu kiasi cha Sh.Milioni 700.
“TBA mmekuwa na matatizo katika maeneo mengi sana kama hamuwezi mtuambie muendelea na kazi mnazopewa na serikali kuu, sisi huku serikali za mitaa mtuache tuwape watu wengine, wapo watu wanajengaa vizuri na kwa wakati kuliko nyinyi tutawapa hata Suma JKT ambao pia wanao watu katika kazi kama hizi,” – Jafo
Jafo ameitaka TBA kukamilisha majengo hayo haraka kabla ya mwezi Februari mwaka 2018 kwani viongozi wa wilaya wanateseka kwa kukosa makazi na Ofisi na pia ujenzi wa shule Kongwe walizopewa watoto, wanakosa miundombinu bora.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA DECEMBER 29 2017? UNAWEZA KUANGALIA HAPA CHINI