Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel amekagua mradi wa Karakana ya Mafunzo ya Ufundi eneo la Magogo Geita uliofadhiliwa na mgodi wa Dhahabu Geita ni baada ya kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi aliyoiunda kufatilia utekelezaji wa fedha za miradi ya jamii zinazotolewa kila mwaka na GGM kwa asilimia moja ya mapato yao kwa mwaka.
RC Robert amebaini mapungufu kwenye mradi huo na amewakataa Watendaji wanaoiwakilisha Serikali ya mkoa huo kutoa maamuzi kwenye fedha zinazotolewa na GGM kuchangia maendeleo ya jamii na kutoa maagizo kwa vyombo vya Dola kuwachunguza Watendaji walioshiriki kwenye kuweka makubaliano kwenye mradi huo.
MAZISHI JUMATATU: BADO HAIJULIKANI NI DINI GANI ITAMZIKA MZEE KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA