Mbunge wa Jimbo la Starehe Charles Kanyi maarufu Jaguar amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya kufuatia matamshi aliyotoa akitaka Watanzania na Waganda wanaoishi nchini Kenya waondolewe ndani ya Saa 24 la sivyo watawaondoa kwa nguvu.
Jaguar amekamatwa na Maofisa wa Polisi waliokuwa wamevaa kiraia mida Saa sita na nusu leo akiwa nje ya ukumbi wa Bunge la Kenya. Hii inafuatia matamshi aliyotoa akiwa katika eneo la Kirinyaga ambapo Wafanyabiashara walilaumu wageni kuingilia biashara zao.
“Ikiwa unatathmini masoko yetu, Wauganda na Watanzania wamechukua biashara zetu … Sasa tunasema kutosha ni ya kutosha. Ikiwa mwisho wa saa 24 haitoshi kwa kuwafukuzwa, tutawaondoa na tutawapiga na hatuogopi mtu yeyote, “alisema Njagua.
Via Citizen TV