Leo March 2, 2018 Nakusogezea stori kutoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili Habinder Seth na James Rugemalira umedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola 22.198 Milioni za Marekani (Sh309.5 Bilioni) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mwendesha mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai amedai hayo mahakamani leo March 2, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati shauri lilipotajwa.
“Upelelezi wa kesi hii bado haujakamilika, hivyo tunaomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa,” -Swai.
Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 16, 2018 itakapotajwa. Washtakiwa wamepelekwa rumande.
Naibu waziri alivyomfungia Roma leo na kumpa onyo Nay wa Mitego