AyoTV

VIDEO: Kauli ya serikali kuhusu waliohusika na mauaji ya wakulima na wafugaji

on

Serikali imeagiza wahusika wote wa mauaji ya wakulima na wafugaji nchini wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo, kauli hiyo imetolewa bungeni leo September 15 2016 na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mikumi Joseph Haule aliyehoji mkakati wa serikali kukabiliana na mauji yanayoendelea jimboni kwake.

Waziri Nchemba amesema…>>>’Hakuna shamba wala mifungo inafanana na thamani ya mwanadamu, naagiza wahusika wa mauaji wakamatwe haraka na kuwekwa ndani

Kama magereza zimejaa basi waachiwe vibaka wa simu kisha wauaji wawekwe ndani ili tukomeshe vifo vya watu wasio na hatia‘ –Waziri Nchemba

Unaweza kuyapata yote kwenye hii video hapa chini…

ULIMIS MANENO YA PROFESA TIBAIJUKA BAADA YA KWENDA KUSHUHUDIA TETEMEKO LA ARDHI

Soma na hizi

Tupia Comments