Leo April 27, 2018 nakusogezea stori kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba ambapo amechukua muda wake kuandika zaidi ya maneno 2000 kuhusu wimbo wa Taifa na ramani ya Tanzania.
Katika ukurasa wa Facebook wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania , Makamba amechukua maoni ya watu mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na viongozi wengine na kutolea ufafanuzi katika andiko hilo lililochapishwa siku moja baada ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Nanukuu baadhi ya aliyoyaandika Makamba “Katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, ambazo nilishiriki kama Msaidizi wa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Ndugu Jakaya Kikwete, hoja ya uzalendo na urithi wa Mwalimu Nyerere kwa taifa letu ilichukua nafasi kubwa”
“Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA kwenye uchaguzi ule, Freeman Mbowe, katika mikutano yake ya kampeni, alimtaja sana Mwalimu Nyerere, alitumia sana bendera ya taifa na alikuwa akiwaimbisha wananchi wimbo wa taifa” -Makamba
“Hata hivyo, katika kuimbisha wananchi wimbo wa taifa, aliwaeleza kwamba wimbo huo umekosewa kwenye mpangilio wa beti, kwamba ubeti wa pili ulipaswa kuwa ndio ubeti wa kwanza. Kama mnavyofahamu, kwenye mstari wa kwanza kabisa wa wimbo wetu wa taifa, tunamuomba Mungu aibariki Afrika” -Makamba
“Ubeti mzima wa kwanza wa wimbo wetu wa taifa unahusu Afrika. Tanzania tunaikumbuka kwenye ubeti wa pili. Afrika imetajwa mara tano kwenye wimbo wetu” -Makamba
“Hoja ya Ndugu Mbowe ilikuwa ni kwamba lazima tuwe wazalendo kwa kuiweka Tanzania mbele. Kwahiyo, lazima ubeti wa pili unaoanza na “Mungu Ibariki Tanzania” uwe ndio ubeti wa kwanza. Watu wengi, hasa vijana, wakawa wanaona mantiki katika hoja yake” -Makamba
“Hata hivyo, baadhi yetu katika timu ya kampeni ya CCM tukaona kwamba Mbowe amekosa uelewa wa msingi muhimu wa kutafuta uhuru wetu na kujenga taifa letu. Tukaamua kumjibu tukieleza kwamba haelewi historia ya Tanzania wala urithi wake” -Makamba
“Tukatoa sababu. na mjadala wa mpangilio wa beti za wimbo wetu wa taifa ukafa. Hata hivyo, wakati tunaadhimisha miaka 54 ya Muungano wetu, ambao ni utambulisho wa nchi yetu, kielelezo cha utaifa wetu, na kilele cha umoja wetu, ni muhimu kukumbushana kidogo.” -Makamba
Kusoma andiko lote lililoandikwa na Mbunge wa Bumbuli ambae ndie Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, unaweza soma hapa chini