Kiungo na nahodha wa FC Barcelona Andre Iniesta leo ameamua kutangaza maamuzi magumu katika maisha yake ya soka baada ya kuthibitisha kuwa ataondoka FC Barcelona msimu huu, Iniesta ametangaza kuwa ataondoka FC Barcelona baada ya kuichezea club hiyo kwa misimu 16.
Iniesta hadi atangaza leo hii kuwa ataondoka FC Barcelona amefanikiwa kuichezea jumla ya game 669, akifunga magoli 57 na kushinda mataji 31 kama taji la UEFA Champions lakini pia amefanikiwa kutwaa makombe matatu akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania.
Andre Iniesta mwenye umri wa miaka 33 kwa sasa ametangaza maamuzi hayo na sasa anahusishwa kwenda kucheza Ligi Kuu Chini lakini kwa upande wake hajathibitisha chochote kama msimu hujao atakuwa uwanjani au ndio anaachana na soka jumla.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao