BAADHI ya wafugaji wa Vijiji vya Nyakenge na Kizapara katika Kata ya Mkamba wilayani Mkuranga, Pwani wamesimulia jinsi walivyovamiwa na mifugo yao kuchukuliwa huku wakiiomba Serikali kuwasaidia kupatikana kwa mifugo yao zaidi ya 127.
Wafugaji hao wamesema mifugo yao hiyo ilichukuliwa August 17, 2017 baada ya watu wanadaiwa kuwa Askari kuwavamia wakiwa na magari matatu wakiongozwa na viongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mkuranga .
Aidha, wafugaji hao wameiomba Serikali kuwasaidia kupata mifugo yao na iwaelekeze maeneo ya malisho pamoja na kuwaachia huru baadhi ya wenzao wanaoshikiliwa kwa siku tatu sasa.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga amekiri kuwepo kwa oparesheni lakini amekanusha kuchukuliwa idadi hiyo ya mifugo na kubainisha kesho watakutana na wafugaji ili wachague moja kati ya kulipa faini au kupelekwa Mahakamani.
Mbunge Msukuma kamjibu Tundu Lissu kuhusu Bombardier…