Breaking News

BREAKING: Mbunge Ester Bulaya amelazwa baada ya kuugua akiwa rumande

on

Taarifa iliyonifikia usiku huu kutoka Tarime mkoani Mara ni kuwa Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya amewahishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya kuugua akiwa rumande ambako alikuwa ameshikiliwa na Polisi baada ya kumkamata akiwa Hotelini, Tarime.

Katibu wa Mbunge Tarime Vijijini, John Heche, Mrimi Zabron amesema Bulaya anasumbuliwa na kifua ambacho kimesababisha ashindwe kuzungumza lakini hata hivyo Madaktari wanaendelea na matibabu.

Ayo TV na millardayo.com zinafuatalia kwa karibu na zitakujuza zaidi kadiri taarifa zitakavyopatikana.

CHADEMA imethibitisha Ester Bulaya kukamatwa na Polisi…

“Tumuombee Rais Magufuli maana sisi ndio tuliomuajiri…” – Matiko!!!

Kitu Mbunge Heche amesema kuhusu Polisi kukamata Wabunge wa CHADEMA…tazama hapa chini kwenye hii video!!

Soma na hizi

Tupia Comments