Moja ya stori kubwa zilizopewa uzito katika Magazeti ya Tanzania leo August 24, 2017 ni pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Shinyanga kuanza kusikiliza kesi ya jinai inayomkabili Steven Samwel ambaye alijifanya Ofisa Usalama wa Taifa.
Polisi Kigoma inamshikilia mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Paul Shishi ambaye ni Mkazi wa Biharamulo, Kagera kwa tuhuma za kukutwa na noti 63 za bandia ambazo zina thamani ya Tsh. 630,000.
Mahakama ya Wilaya Kahama Shinyanga imeanza kusikiliza kesi ya jinai inayomkabili Steven Samwel aliyejifanya Ofisa Usalama wa Taifa #NIPASHE
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Polisi Kigoma inamshikilia Paul Shishi Mkazi wa Biharamulo, Kagera akituhumiwa kukutwa na noti bandia zenye thamani ya Tsh 630,000 #NIPASHE.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Tarehe kama ya leo 1853, Chips ya kwanza ya viazi iliandaliwa kwa mara ya kwanza na mpishi George Crum wa Marekani. #MWANANCHI.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imesema TANROADS imefanya kosa kupuuza amri ya Mahakama kwa kubomoa nyumba ilizoziwekea kinga. #MWANANCHI.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
"Mfumo wa utozaji kodi nchini si rafiki kwa sababu tunataka kutoza kodi hata kabla uzalishaji haujaanza…" – Peter Serukamba. #MTANZANIA.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
"Tujiandae kuwa na jamii ambayo haitakuwa na vyombo vya habari." – Jenerali Ulimwengu. #MTANZANIA.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Madiwani watatu wa CHADEMA Iringa Mjini wameandika barua kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo kujiuzulu nafasi zao kuanzia jana. #MTANZANIA.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Upelelezi kesi ya shambulio inayomkabili Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea haujakamilika, kesi imeahirishwa hadi Sept 4, 2017. #TANZANIADAIMA.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ameshindwa kuthibitisha Mahakamani iwapo mkojo alioupima ni wa Manji au Askari #TANZANIADAIMA
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Mkumbo amesema Upinzani unapata nguvu mpya kutokana na kujengeka taswira kuwa wanaonewa. #TANZANIADAIMA.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Mfanyabiashara Yusuf Manji kesho atajua hatma yake kama ana kesi ya kujibu au la katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili. #UHURU.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa Tsh. Trilioni Moja kutoka Serikali ya Uingereza kwa ajili ya kuboresha miradi ya maendeleo. #UHURU.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Magazeti na machapisho yote yametakiwa kusajiliwa upya ili kukidhi matakwa ya kanuni ya 17 ya Sheria ya huduma za Habari ya 2017. #UHURU.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Watanzania waishio nje ya nchi wametakiwa kuwa wazalendo kuchangia maendeleo ya nchi baada ya serikali kutangaza fursa za uwekezaji. #UHURU.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Mtoto Shukuru aliyekuwa anakunywa mafuta ya kupikia na sukari amerudishwa Hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake kubadilika ghafla #UHURU
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana walitumia saa tatu kufanya upekuzi nyumbani kwa Mbunge Tundu Lissu, Tegeta. #UHURU.
— AyoTV (@ayotv_) August 24, 2017