Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ndani ya kipindi cha miezi miwili tangu achaguliwe na kuthibitishwa na Bunge kwa kula kiapo kuongoza watu wa Jimbo lake, amethibitisha kuwa ana njaa na kuhakikisha Jimbo lake linakuwa pazuri.
Kama utakumbuka wiki moja iliyopita nilikusogezea stori ya Mbunge huyo kuthibitisha kwamba milioni 90 zake anazopewa na Serikali kwa ajili ya kununulia gari la Mbunge anazigawanya, milioni 45 zinaenda kusomesha yatima na nyingine 45 zinaenda kununua vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya Meru.
“Nilifanya ziara Hospitali ya Meru nikaona kuna wanawake wanalala wawili wawili kwenye kitanda kimoja kutokana na uhaba uliopo, nikajitolea sehemu ya pesa za gari langu nitoe milioni 45 kwa ajili ya kusaidia kupatikana vifaa tiba na vitanda pia“- Mbunge Joshua Nassari.
Sentensi zake nyingine hizi hapa >> “Malengo yangu kwa awamu ya kwanza ni kununua vitanda zaidi ya 200, baada ya muda kidogo nitaangalia kama nitamega sehemu ya mshahara wangu au kwa kushirikiana na wadau ili tuongeze vifaa tiba“-Joshua Nassari.
Huu ni mwanzo tu wa safari yake ya miaka mitano kwenye kiti chake cha Ubunge, mipango inaanzia hapo na kuendelea hivi >>”Naamini ndani ya miaka hii mitano nitaongeza ambulance nyingine kurahisisha huduma kwa wananchi… Nimekuja kuvinunua China ni bora zaidi kwa sababu kuna viwanda vingi, nimeona nikija mwenyewe nitavinunua kwa bei rahisi zaidi tofauti na kununua kwa mfanyabiashara“- Joshua Nassari.
Kama kumbukumbu zako ziko sawa pia utakumbuka ishu ya Rais Magufuli kubadilishia matumizi pesa zaidi ya milioni 200 zilizoandaliwa kwa sherehe ya Bunge akaagiza zikanunulie vitanda hospitali ya Muhimbili, video yake hii hapa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.