Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na club ya Chelsea ya England John Obi Mikel amefikia hatua ya kuvunja mkataba wake na club yake ya Trabzonspor ya nchini Uturuki.
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku chache zimepita toka kiungo huyo atupe lawama wa shirikisho la soka nchini Uturuki kwa kushindwa kusimamisha Ligi wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.
Obi anadaiwa kuwa Jumapili ya March 16 2020 zikiwa Ligi mbalimbali duniani zimesimama kwa hofu ya corona, anadaiwa kuwa aligoma kucheza katika mchezo dhidi ya Basaksehir.
Sababu rasmi za kuvunjwa kwa mkataba huo hazijawekwa ila Obi hatopokea fidia yoyote kwani yeye ndio aliyeomba, hadi sasa zaidi ya wachezaji watano Wakubwa Ulaya wamethibitika kupata maambukizi.