Julai 5, 2023 Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga alipost video clip ikimuonesha Shukurani Balitima ikiwa kama sehemu ya kuvutiwa na maneno ya Mkulima huyo ambae alisikika katika video clip hiyo akishukuru kutosheka na Ugali kwa mboga ya Majani ya Maboga.
Joseph Kusaga baada ya kupost video clip hiyo aliambanitanisha na maneno yanayosomekana hivi namnukuu…‘Thamini vitu rahisi, kwa kuwa ndivyo utajiri wa kweli wa maisha.🌽 Furaha sio kuwa na vyote, ni kuthamini kile ulicho nacho. Kwa sahani ya UGALI na mioyo iliyojaa upendo, sisi ni matajiri kuliko tulivyowahi kufikiria. Video ya mtu huyu na binti yake Rehema.. inatia moyo sana kwa unyenyekevu wake. Ningefurahi kukutana nao siku moja—unyenyekevu wao na neema ni funzo kwetu sote”
Sasa baada ya Mkurugenzi kueleza kila alichovutiwa Hatimae Hussein, producer wa #Leotena ya @cloudsfmtz @praf.paparaz amempata mwananchi huyo ambaye ni mkazi wa Kaliua mkoa wa Tabora akiwa tayari amepata taarifa hizi na ana furaha ya kukutana na Big Joe.