Ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa na wengi hasa wapenzi wa mchezo wa ngumi duniani, imewadia ambapo tambo na majigambo ya nani ni nani yatafika mwisho baada ya pambano la ngumi lililokuwa linatajwa kwa muda mrefu kumalizika.
Ni usiku wa Jumamosi April 29, 2017 katika uwanja wa Wembley jijini London kutashuhudiwa pambano kali la ndondi litakalowakutanisha miamba wawili kutoka Uingereza na Ukraine, Anthony Joshua vs Wladimir Klitschko.
Kuelekea pambano hilo kumekuwa na tambo nyingi kutoka kwa mabondia hao ambao kila mmoja ametamba ataibuka kidedea dhidi ya mwenzie. Na kwa kuwa nafahamu nina watu wanaoupenda mchezo huo, basi hizi hapa baadhi ya dondoo muhimu kuzifahamu kuelekea mchezo huo. Pambano hilo litapigwa mbele ya mashabiki wanaokadiriwa kufikia 90,000 katika uwanja wa Wembley mjini London.
Umri
Antony Joshua ana umri wa miaka 27 wakati mpinzani wake Wladimir Klitschko ana umri wa miaka 41, ikiwa namaana kuwa anapanda ulingoni akiwa amezidiwa miaka 14 na mpinzani wake lakini wa urefu sawa wa futi 6 na inchi 6.
Kiasi cha fedha watakachopata
Kwa mujibu wa The Sun, pambano hili litawaingizia fedha kiasi cha pound 15 million kila mmoja bila kujali kushinda au kupoteza na ni pambano ambalo linakadiriwa kuvunja rekodi ya kuingiza watazamaji wengi zaidi Uingereza huku likitarajia kuingiza zaidi ya paundi 50 million – na kulifanya pambano ghali zaidi Uingereza.
Mapambano waliyocheza
Wladimir Klitschko anaingia ulingoni akiwa amecheza mapambano 68 ambayo ameshinda mapambano 64 huku mapambano 53 akishinda kwa ‘KO’. Hii ina maana kuwa amepoteza mapambano manne pekee huku pambano la mwisho kupoteza ilikiwa 2015 dhidi ya Tyson Fury ambalo alipoteza kwa pointi baada ya round 12. Hii ni baada ya kujiunga na ngumi za kulipwa baada ya kutwaa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olympic 1996 mjini Atlanta.
Kwa upande wa Antony Joshua tangu alipotwaa medai ya dhahabu kwenye mashindano ya Olympic London mwaka 2012 alijiunga rasmi na ndondi za kulipwa ingawa hajacheza mapambano mengi – amepigana mara 18 ambapo ameshinda yote kwa KO.
VIDEO: Dr Dre alivyompigia video call bondia Anthony Joshua. Bonyeza play kutazama…
Dr Dre kampigia simu bondia Anthony Joshua kabla ya pambano la kesho vs Klitschko na kumtakia kila la kheri #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/0g90UQcHqz
— millardayo (@millardayo) April 28, 2017