Ni habari kubwa na ya kwanza kutoka IKULU Dar es salaam leo yakiwa ni maamuzi mengine ya Kiongozi wa Nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ambapo uteuzi huu unaanza leo tarehe 26 March 2019.
Taarifa ya IKULU mapema hii imesema Rais JPM amemteua Mhandisi Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na anachukua nafasi ya Richard Mayongela ambae uteuzi wake umetenguliwa na anatakiwa kuripoti Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambako atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Ndyamukama alikuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam na ndiye alikuwa msimamizi Mkuu wa ujenzi wa majengo namba 3 (Terminal 3) ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam ambayo yapo katika hatua za mwisho kukamilika
VIDEO: TAIFA STARS NA MWAKINYO WALIPOITWA NDANI YA IKULU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
VIDEO: WATU WAANGUA VICHEKO IKULU, MANARA AKIMWAMBIA RAIS MAGUFULI IPO SIKU UTAWAITA SIMBA IKULU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA