Leo September 6 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatembelea wakazi wa Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam ambao nyumba walizokuwa wakiishi katika eneo hilo zilivunjwa mwaka 2012 kwa makubaliano ya kujengwa nyumba za kisasa na kuwaahidi kuwa Serikali itaanza kujenga nyumba hizo katika kipindi cha Miezi miwili kuanzia sasa.
Rais Magufuli amesema ujenzi wa nyumba hizo utakamilika katika kipindi cha mwaka mmoja na baada ya hapo Wakazi wote 644 walioondolewa kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa watapatiwa nyumba za kuishi na kwamba wataishi katika nyumba hizo kwa muda wa miaka mitano bila kulipa pango na baada ya muda huo kuisha wataandaliwa utaratibu wa kila mmoja kuuziwa nyumba anayoishi.
>>>”Nakwenda kutoa pesa Mwezi huu, ili Mkandarasi atakayeteuliwa aanze kujenga nyumba za wakazi wote 644, wakati wanapojenga hayo majengo ya wakazi 644, ujenzi utaendelea pia katika maeneo mengine, ili kusudi kama yanajengwa maduka makubwa (Shopping Malls) au zinajengwa nyumba zingine za wananchi wanaohangaika nao tuwalete hapa’-JPM
Pamoja na kumpongeza kwa kazi nzuri anazofanya, Rais Magufuli amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Shirika na Nyumba la Taifa (NHC) Neemia Mchechu Kyando kuwaondoa wapangaji ambao ni wadaiwa sugu wa pango zikiwemo Taasisi za Serikali ambazo amezipa siku saba kuwa zimelipa madeni yao.
>>>”Wale wapangaji wote lazima walipe madeni yao, nimetoa maagizo leo, wapangaji wote wa Serikali, Wizara ya Ujenzi, Wizara gani kule… ndani ya siku saba lazima wawe wameshalipa madeni yao wasipolipa endelea kuwatoa nje’-JPM
“Endelea hivyo hivyo usiogope kumtoa nje mtu yeyote, awe amepangishwa ni wa CCM mtoe nje, awe wa UKAWA mtoe nje, awe Serikali mtoe nje, awe Waziri Mtoe nje, mpangaji huyo awe ni Rais mtoe nje, ni lazima upate pesa zitakazowezesha kuendesha Shirika la Nyumba la Taifa” Amesisistiza Rais Magufuli’-JPM
ULIKOSA MAAGIZO HAYA YA RAIS MAGUFULI KWA WAKAZI WA MAGOMENI KOTA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI