Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeita Waandishi leo Dar es salaam na kutoa onyo kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ambae alipeleka ushahidi wa tuhuma za Madiwani wa CHADEMA kupewa rushwa ili wahamie CCM Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola amesema “Ni kama Mh. Nassari na wenzie wanataka kulifanya hili swala kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria, namuonya Mh. Nassari”
“Ameshaleta taarifa yake kwetu, atuachie tufanye kwa mujibu wa sheria na sio kutushinikiza kama kauli aliyoitoa jana….. nitaendelea kutoa series, hii Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu tutachukua hatua za kisheria dhidi yake”
Unaweza kutazama tamko zima lililotolewa na TAKUKURU ikiwemo kwanini hawajaenda Mahakamani kwa haraka kwa kubonyeza play kwenye hii video hapa chini
VIDEO: Makomando wa Tanzania wakionyesha uwezo, waruka kwenye gari na kuonyesha uwezo wao… tazama kwenye hii video hapa chini.
UNATAKA KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI? Breaking NEWS, Za Mastaa, Siasa, Michezo na nyingine…. fanya jambo moja tu rahisi… BONYEZA PAGE ZIFUATAZO ili nikutumie kila kitu kiganjani mwako >>> INSTAGRAM <<<< FACEBOOK >>>> TWITTER >>> APP MPYA YA MILLARD AYO pia bonyeza SUBSCRIBE HAPA >>> YOUTUBE