Tunayo story kutokea kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambapo imewapatia vyeti wanafunzi 25 wa Shule ya Sekondari ya Kondo baada ya kuhitimu mafunzo ya kiingereza kupitia mpango wao wa Access.
Akizungumza na Ayo Tv, Afisa wa Masuala ya Umma wa Ubalozi wa Marekani Ms.Brinille Ellis amesema wanafunzi hao wametunukiwa vyeti hivyo baada ya kuhitimu mafunzo ya kiingereza yanayosimamiwa na Ubalozi wa Marekani.
“Wanafunzi hawa wameonyesha jinsi walivyofanya vizuri katika masomo yao na ndio maana wamepatiwa vyeti, mafunzo haya yatawasaidia katika mambo mengi ikiwemo hata kwenda kusoma Marekani masomo wanayoyahitaji,“amesema.