Club ya Man United chini ya kocha wake mkuu Ole Gunnar Solkjaer imesafiri kuelekea Norway kucheza mechi za kirafiki na kufanya maandalizi yao ya mwisho ya kuanza kwa msimu mpya wa 2019/2020 wa Ligi Kuu England, Man United wamesafiri bila uwepo wa mshambuliaji wao Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 26.
Kocha Ole Gunnar Solskjaer amemuacha Lukaku katika jiji la Manchester kikosi kikiwa katika safari hiyo kutokana na kudaiwa hayupo kwenye mpango wake wa msimu ujao, kwani staa huyo raia wa Ubelgiji anakaribia kujiunga na club ya Juventus ya Italia, hivyo wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wake wanaafikiana ada ya uhamisho tu.
Man United itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kristianund, Juventus wanaripotiwa kuwa tayari kutoa kiasi cha pound milioni 53.9 pamoja na Paulo Dybala ili kumpata Lukaku, Lukaku ataondoka England na kwenda kucheza Italia baada ya kucheza EPL kwa miaka 8 toka alipojiunga na Chelsea 2011 akitokea Anderletch ya kwao Ubelgiji, 2014 West Bromwich kwa mkopo, Everton halafu Man United.
VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6