Ikiwa zimepita siku mbili baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kucheza game yake ya kwanza ya fainali za AFCON 2019 na kupoteza mchezo kwa magoli 2-0 dhidi ya Senegal, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike amewaita waandishi wa habari leo na kueleza kuwa watu wanapaswa waelewe hakuna timu iliyokuja hapa kufungwa.
“tunaenda kucheza na Kenya ambao ni ndugu zetu tunazungumza nao lugha moja kiswahili ila kwa sasa tunatakiwa kujenga wachezaji namna ua kushinda namna ya kupambana na kuamini katika wao, huwezi kutabiri kitu katika mpira malengo yetu ni kufanya vizuri, nakuhakikishia hakuna timu iliyokuja hapa kwa ajili ya kupoteza”>>> Amunike
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars mchezo ujao utachezwa dhidi ya timu ya taifa ya Kenya ambayo nayo imetoka kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria kwa magoli 2-0, kwani yoyote kati ya Kenya na Tanzania akipoteza mchezo huo ni wazi atakuwa ameaga mashindano hayo kwa asilimia kubwa au asubiri baraka za Best Looser.
VIDEO: Inabidi Muielewe tu Taifa Stars, Msuva Kaongea Kwa Hisia